Tuesday, July 19, 2016

The Game awatafuta wabaguzi wa rangi

http://richestcelebrities.org/wp-content/uploads/2015/04/The-Game-Net-Worth.jpg
RAPA Jayceon Taylor ‘The Game’, amedai kwamba anawatafuta wabaguzi wa rangi ambao wamemuua kaka yake Spanky bila sababu za msingi.
Spanky amekuwa miongoni mwa watu ambao wameuawa mwaka huu kutokana na ubaguzi wa rangi ambao unaendelea nchini Marekani.
The Game, amedai kwamba alikuwa na Spanky tangu wakiwa wadogo katika jiji la Los Angeles, hivyo ameguswa na kifo hicho na amepanga kuwatafuta waliohusika na tukio la kifo hicho.
“Inashangaza kuona hali hii ikiendelea, binadamu wote ni sawa lakini cha kushangaza kuna watu wengine wanajiona kuwa wao ndio sahihi kuishi, nimeumia sana kuona rafiki yangu wa karibu kama kaka yangu akiuawa bila sababu, nitahakikisha napambana na watu ambao wamefanya tukio hilo,” alisema The Game.

No comments:

Post a Comment