Tuesday, July 19, 2016

Shaa adai alirudia video ya Sawa,baada ya Chura ya Snura kufungiwa.

Msanii wa kike wa Bongo Fleva,Shaa amefunguka na kusema kuwa ilimlazimu kurudia video ya wimbo wake mpya ‘sawa’ baada ya BASATA kufungia video ya Chura ya mwanadada Snura.
Shaa amesema kuwa uamuzi huo ulikuja baada ya kuwepo kwa picha tata kwenye video hiyo ambazo hawakuzikusudia kutokana na mazingira ya uchukuaji wa picha hizo.
Video ya sawa tuliimaliza kitambo sana,lakini baada ya video ya chura kufungiwa ilitufanya tufikirie mara mbili kwa sababu kulikuwa na shots ambazo mtu unaonekana paja na vitu vitu kama hizo ambazo hatukuzi shoot makusudi,ikabidi nimrudishie video Justin Campos ,tukarudia zaidi ya asilimia 50 ya shotz” alisema Shaa kwenye mahojiano yake na HZB TV.

No comments:

Post a Comment