Msanii wa Hip hop Tanzania Kala Jeremiah amedai kuwa vyombo vya habari vimechangia kwa kiasi kikubwa wasanii wa bongo fleva kuacha kuimba nyimbo zenye ujumbe kama ilivyokuwa zamani.
Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5 Kala amedai kuwa radio nyingi zinaendeshwa kibiashara zaidi kuliko kuangalia maisha kitu ambacho yeye anakilaani kwani vyombo vya habari vina kazi ya kuelimisha pia.
“Wasanii wengi siku hawatoi nyimbo zenye ujumbe mzito kwa sababu promotion ya nyimbo kama hizo sio kubwa,yaani hazizunguki sana..mfano feruzi angetoa wimbo wake wa ‘starehe’ kipindi hiki asingepata air time kwa sababu tu mtu wa radio angeona kupiga wimbo ni kufanya tangazo la ukimwi kitu ambacho kinapotosha watu wengi” amefunguka Kala ambaye yuko mbioni kuachia wimbo wake mpya wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment