Tuesday, July 19, 2016

Alichojibu Richard wa Big Brother baada ya kuombwa amshauri Idriss Sultan ,hiki hapa.

Mshindi wa Big brother II mwaka 2007 Richard Bezuidenhout ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akiishi nchini Canada amekuja Tanzania kutambulisha filamu yake mpya na amekuwa akifanya media tour kuitangaza fialmu hiyo.
Kwenye moja ya mahojiano yake na Sam Misago staa huyo wa Big Brother aliulizwa kuwa angependa kumshauri nini Idriss ambaye pia ni mshindi wa Big Brother ambaye amekuwa akisakamwa na vyombo vya habari kuwa ametumia vibaya pesa alizoshinda Big Brother.
Kama kuna ushauri ninaweza kumpa Idriss itakuwa on personal basis,siwezi kukaa hapa mbele za watu na kuanza kumshauri itakuwa sio poa,sitaki ionekane kama ninam diss kwa sababu mimi mwenyewe bado kijana tuna exprience life in different level,so one day we shall sit down to exchange one or two things” alisema Richard

No comments:

Post a Comment